SHIRIKA la Maendeleo la Restless limewataka wanafunzi wanaohitimu vyuoni kuwa na mtazamo tofauti ikiwamo wa kujiajiri kuliko kutegemea
ajira kupunguza tatizo la ajira nchini. Akizungumza na RAI, Meneja wa Maendeleo Restless, Nicas Ngumba alisema lengo la kuanzisha program hiyo ni katika juhudi za kupunguza tatizo la ajira nchini.
Ngumba alisema baada kufanya uchunguzi imebainika kuwa wapo vijana wengi wanaomaliza elimu ya vyuo na hawana kazi.
Alisema shirika hilo linatoa mafunzo ya ujasiriamali katika kuongeza kipato katika jamii, afya na jinsi ya kupata haki zao katika suala zima la upatikanaji wa ajira kwa vijana wanaoendelea na masomo katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
“Kwa wale vijana wanaojiunga na programu hii tunachukua watu 34 ambao wanafanya kazi kwa kujitolea na katika hao watu 17 ni kutoka Uingereza na 17 ni kutoka Tanzania,”alisema Ngumba.
Alisema waajiri wengi wanataka watu wenye uzoefu usiopungua miaka mitatu na zaidi jambo ambalo limekuwa chagamoto kubwa ya vijana wengi wanaotoka vyuoni hivyo kukosa ajira nchini.
Naye Ofisa Uhusiano wa benki ya Exim, Cosmas Nade alisema benki hiyo inatoa ajira kwa vijana wengi wanaohitimu vyuoni na kuwafundisha jinsi ya kufanya kazi
“Kwa mwaka tunafungua matawi matatu/manne na kuwaajiri vijana 80 hadi 100 wenye uzoefu na wasiokuwa na uzoefu.
“Hivyo tunachukua watu 40 kutoka vyuoni na 40 ambao wana uzoefu katika kazi,” alisema Nade
Source: Mtanzania

No comments:
Post a Comment